Friday 26th April 2024
logo

TUME YA UTANGAZAJI ZANZIBAR YASISITIZA MWONGOZO WA HUDUMA ZA UTANGAZAJI KUFUATWA KIKAMILIFU

Mhandisi Mkuu wa Tume ya Utangazaji Zanzibar, Ali Hussein Ayoub akisisitiza jambo katika semina ya siku moja kuhusu mwongozo wa Huduma za Utangazaji wakati wa Uchaguzi, 2020 iliyowashirikisha wamiliki wa vyombo vya Utangazaji Zanzibar, iliyofanyika katika Chuo Cha Utalii Zanzibar, huko Maruhubi.

TUME ya Utangazaji Zanzibar imefanya mkutano na wamiliki wa vyombo vya Utangazaji Zanzibar kuhusu mwongozo wa huduma za utangazaji wakati wa Uchaguzi, 2020.
Afisa sheria kutoka Tume ya Utangazaji Zanzibar Khadija Mabrouk ametoa tahadhari kwa mtu yoyote kutangaza matokeo ya uchaguzi kwa njia yoyote kabla kutangazwa rasmi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), na kuzitaja adhabu ya kosa hilo kwa mujibu wa aina ya mtu au taasisi.
Akifafanua sheria nambari 4 ya mwaka 2018 kifungu cha 127(1) a,b,c alisema “ni marufuku kwa mgombea, chama cha siasa, taasisi mtu mwengine yoyote , kutangaza matokeo ya uchaguzi kwa njia yoyote ya mawasiliano kabla ya kutangazwa rasmi na Tume”, alisema Mwanasheria.
Alifafanua sheria hiyo na kusema mtu, iwapo matokeo hayo yatatangazwa kabla ya kutangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar , atakua ametenda kosa na akitiwa hatiani atapata adhabu kali .
Akizitaja adhabu hizo ni pamoja na kwa mgombea kutumikia kifungo kwa muda usiopungua shilingi milioni hamsini na hatoruhusiwa kugombea katika uchaguzi kwa kipindi cha miaka kumi.
Mwanasheria pia alisema ikiwa chama cha siasa au taasisi , adhabu isiyopungua shilingi milioni mia moja na ikiwa mtu mwengine atatumikia kifungo kisichopungua miezi thelathini.
Semina kwa wamiliki wa vyombo vya Utangazaji Zanzibar imeandaliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa lengo la kuwapa uelewa wanahabari juu ya kuufuata Mwongozo wa Huduma za Utangazaji wakati wa Uchaguzi, 2020.
.

Other Top Story