
Katibu Mtendaji
Tume ya Utangazaji Zanzibar
Ujumbe wa Katibu Mtendaji
Ujumbe wa Katibu Mtendaji
Napenda kuchukua fursa hii kutoa salamu za dhati na pongezi kwa kazi kubwa inayofanywa na Tume ya Utangazaji Zanzibar katika kusimamia, kuratibu na kuendeleza tasnia ya utangazaji nchini. Tume imeendelea kuwa nguzo muhimu katika kuhakikisha kuwa huduma za radio, televisheni na majukwaa ya kidijitali yanatoa taarifa sahihi, zenye weledi, na zinazozingatia misingi ya maadili, sheria na maslahi ya umma.
Ninatoa wito kwa vyombo vyote vya habari kuendelea kushirikiana kwa karibu na Tume ya Utangazaji Zanzibar katika kutekeleza majukumu yake ya kisheria, hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linaendelea kusonga mbele katika mageuzi ya kiuchumi, kijamii na kiteknolojia. Ushirikiano wenu ni muhimu katika kuhakikisha kuwa Zanzibar inabaki kuwa mfano wa utangazaji wenye maadili, heshima, na unaolinda maslahi ya wananchi. Nawashukuru wadau wote kwa ushirikiano na kwa mchango wenu katika kuiwezesha Tume kutimiza majukumu yake kwa ufanisi.
Tume itaendelea kusimamia na kuimarisha misingi ya uhuru wa vyombo vya habari sambamba na uwajibikaji, kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Ahsanteni
Xchange Rate
Habari & Matukio
- All Posts
- Habari
- Matukio

Takiwimu
Majukumu ya Tume y Utangazaji Zanzibar
No Data Found
Tume ya Utangazaji
No Data Found
No Data Found
Washirika Wetu









